Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema migogoro mingi inayotokea katika maeneo ya kijeshi ni kutokana na maeneo hayo kukosa hati na wananchi kuyanunua pasipo kujua historia yake.
Meja Jenerali Mabele amesema hayo katika kikao cha wahariri na waandishi wa Habari Makao makuu ya JKT Leo Machi 01,2023 wakati akitoa taarifa ya kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo yatakayofanyika mwezi Julai mkoani Dodoma yakiambatana nam bio za rida’Marathon’,matibabu na ushauri bure pamoja na maonesho ya bidhaa ambapo amesema maeneo hayo yapo chini ya katibu mkuu wa wizara na yapo kwenye utaratibu wa kupimwa ili kuondoa migogoro hiyo.
“Unaweza ukamkaribisha akasema nitakuwanalimalima mchicha kidogo baadae anajenga kakibanda ka nyasi mwisho wa siku kumtoa pale ni mgogoro na wewe huna hati sasa kinachofanyika wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa limeanzisha mkakati maalumu wa kuhakikisha maeneo yote ya kijeshi yanapimwa na yanakuwa na hati yako maeneo yana hati mengine yako kwenye process ukifuatilia migogoro ilianza anzaje utashangaa mwingine atakwambia nilikuwepo mwingine ana kwambia niliuziwa bila kujua eneo hili nilajeshi” Mkuu wa JKT Meja Generali Rajabu Mabele