Binti huyo alishtakiwa na baba yake baada ya kuripotiwa kuwa hakuacha chuo kikuu ili kumtunza baada ya kujeruhiwa katika ajali ya gari huko Puyang, China.
Mwanamume huyo, aliyejulikana kama Zhang, aliwasiliana na binti yake mara nyingi baada ya kupata ajali ya gari na kujaribu kumshawishi kuacha chuo kikuu ili kumtunza lakini baada ya majaribio kadhaa, mwanamke huyo block nambari ya baba yake ndipo baba akawasilisha malalamiko katika mahakama.
Ombi hilo, aliomba yuan 1,500 ($216) sawa na (tsh laki 4)kwa mwezi kwani Kifungu cha 26 cha Sheria ya Kiraia ya China kinawataka watu wazima wote kuwa na wajibu kamili wa kusaidia na kuwalinda wazazi wao, kama ilivyoripotiwa na Oddity Central.
Zhang alisema alitaka binti yake kusimamisha elimu yake na kumsaidia na binti huyo alielezea kwamba mahitaji yake ya chuo kikuu hayamruhusu kuacha kila kitu haraka na kumsaidia kwani ana ndugu wengine wawili ambao wanaweza kusaidia.
“Sina wakati wa kurudi kumtunza na zaidi ya hayo, nina kaka wawili wakubwa ambao wangeweza kumtunza, kwa hiyo ni lazima nirudi shule nili block nambari ya simu ya baba yangu, lakini kwa sababu tu jumbe zake zote zilikuwa za malalamiko, jambo ambalo lilinifanya niwe na wasiwasi na kuogopa zaidi kuliko kawaida zingefanya nishindwe kusoma na kufanya mitihani nili hisi nimechoka hata zaidi kiakili na kimwili.” Alisema binti huyo akiwa mahakamani hapo.
Maafisa wa mahakama walisikitikia hali ya binti huyo kwa kuwa walibaini kuwa bado alikuwa shuleni na aliweza kumudu malipo ya matibabu na matumizi Lakini walimwambia anapaswa kuwa na uangalizi zaidi kwa hali ya baba yake bila kuacha masomo yake.
Baba yake bado anapanga kukata rufaa!