Watengenezaji maarufu duniani wa nguo za michezo “Puma” walitangaza siku ya jana kuwa kmwa sasa wanashirikiana na chapa ya mwimbaji maarufu Rihanna ya Fenty.
Ingawa kampuni hiyo haikutoa maelezo yoyote ya ziada juu ya muunganiko huo japo wadokeza kuwa “inakuja hivi karibuni.”
Tangazo hilo lilipokelewa na msisimko kutoka kwa mashabiki katika sehemu ya comment ya post hiyo kwenye page ya instagram iliyosema;
She’s back,” Amerudi,” post iliyo ambatana na logo za Fenty na Puma. .
Na wengi walio na ushirikiano na kampuni hiyo walionesha kuunga mkono kurejea kwa Rihanna, , “🔥🔥🔥🔥🔥.”
Rihanna (35) aliunganishwa kwa mara ya kwanza na Puma mnamo 2014 alipochukua kama mkurugenzi wa ubunifu wa chapa ya Ujerumani.
Wakati huo, Rihanna alifanya kazi na Puma kuunda na kubinafsisha mitindo ya kawaida ya Puma na pia kuunda mitindo mipya ya kuongeza kwenye trendings ya bidhaa za Puma,kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.
Kama utakumbuka mwaka 2019, Rihanna alitangaza kuwa anajiunga na LVMH ili kuunda mtindo wake wa Fenty, na kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuongoza jumba la mitindo.
Rihana mwaka 2021 aliachana na chapa hiyo na kufungua kampuni ya nguo za ndani (Savage Fenty) vipodozi pamoja na bidhaa za afya ya ngozi (FENTY skin).
Tangu wakati huo, Rihanna amekuwa bilionea mdogo zaidi wa kike aliyejitengeneza Marekani na kwa sasa anatarajia mtoto wake wa pili na A$AP Rocky.