Msanii nyota wa Pop Justin Bieber ametoa taarifa za kughairi tarehe zake zilizokuwa zimebaki za tour yake ya “Justice World Tour” baada ya kuahirisha kutokana na wasiwasi wa kiafya.
Tarehe hizo ziliondolewa kwenye tovuti rasmi ya Bieber kufikia siku ya jumanne Na ratiba hizo pia ziliorodheshwa “ Ticketmaster” ikiwa ni pamoja na vituo vya California, Connecticut na Washington, D.C. Zimeondolewa pia.
Wawakilishi wa Bieber na Ticketmaster hawakujibu mara moja juu ya hayo kwenye wakutoa maoni.
Mnamo Septemba 2022, beiber alitangaza kupitia Instagram kwamba alikuwa akisisitiza kupumzika kwenye ziara hiyo, ambayo ilianza Februari 2022 na ilikuwa na perfomance 70 zilizopangwa kufanyika 2023.
Beiber anasumbuliwa na ugonjwa uitwao “Ramsay Hunt Syndrome” ambao ni ugonjwa wa neva unaweza hata kusababisha kupooza .
Amemaliza kwa kuwaambia mashabiki zake kuwa muda huu atautumia kufanya mazoezi kutumia dawa na kupona viungo vyake ikiwemo mdomo ili kuweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida vizuri zaidi!