Meya huko Maryland amejiuzulu baada ya kukamatwa kwa makosa 56 ya kumiliki na kusambaza picha chafu za watoto.
Patrick Wojahn, meya wa eneo la College Park, anatuhumiwa kwa kuendesha akaunti ya mtandao wa kijamii iliyomiliki na kusambaza washukiwa wa ponografia ya watoto,polisi wa eneo la Prince George ilisema katika taarifa ya habari.
Mnamo Februari, idara hiyo iliarifiwa na Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Kunyanyaswa kwamba akaunti ya mtandao wa kijamii inayoendeshwa na mtu asiye fahamika ipo katika eneo hilo na ilikuwa ikimiliki na kusambaza ponografia ya watoto.
Wojahn, (47)anadaiwa kuweka/kupakia video hizo Januari mwaka huu, polisi wanasema, na kusababisha wachunguzi kupata hati ya upekuzi wa nyumba yake ambapo walipata simu nyingi za mkononi ,kifaa cha kuhifadhia, tablet na kompyuta kutoka nyumbani kwake jambo ambalo lilipelekea kukamatwa kwake siku ya Alhamisi asubuhi.
Jiji la College Park lilitoa taarifa siku ya Alhamisi, na kutangaza kwamba Wojahn alijiuzulu usiku wa kuamkia siku hiyi baada ya saa za kazi,na kwamba uchaguzi maalum utafanyika ndani ya siku 65 zijazo huku Meya Pro Tem Denise Mitchell akichukua nafasi hiyo.
Kwenye barua yake aliandika ; “Ingawa uchunguzi huu hauhusishi biashara yoyote rasmi ya jiji la aina yoyote, ni kwa manufaa ya jamii yetu kwamba ninajiweka kando nakuwa mtulivu,”.
Baada ya uchunguzi wa awali, Wojahn alikamatwa kwa makosa 40 ya kupatikana na nyenzo za kuwanyanyasa kingono watoto na makosa 16 ya usambazaji wa video hizo.
Wojahn alihudumu kama meya tangu 2015 na alikuwa kwenye baraza la jiji tangu 2007.