Staa na mtunzi wa muziki Billie Eilish, ambaye ana wafuasi milioni 110 kwenye ukurasa wake wa Instagram, ametoa sababu kwa mashabiki zake kuwa kwanini ameamua kufuta programu zote za mitandao ya kijamii kwenye simu yake.
“Nilifuta mitandao yote kwenye simu yangu, ambayo ni mpango mkubwa kwang”
“Kwangu mimi, ilikuwa sehemu kubwa sana na sababu hatujakua/kukuzwa kwa kutumia internet
sikuwa mtoto kwenye matumizi ya iPad, namshukuru Mungu lakini ukweli, ninahisi kama nilikua katika wakati mzuri wa mtandao ambao haukuwa sahihi kwangu na nilikuwa na utoto kama na nilikuwa nikifanya vitu kila wakati,” alielezea.
Billie alisema sababu nyingine ya kufuta programu zake za mitandao ya kijamii ni kwa sababu hapendi kutazama picha zake.
“Mimi ni mtu anayeingia kwenye mtandao na kutobadilisha chochote kuhusu mtu niliye au maisha ninayoishi, na kuendelea tu kufanya kile ninachofanya kwa miaka mingi, na polepole video ambazo ninatazama ninachokiona kwenye mtandao zaidi kwenye comment mfano ;Eww, stinky.’ Sipendi hivyo,”
Eilish amezungumza waziwazi kuhusu kukatishwa tamaa kwake na aibu kuhusu mwili wake huko mtandaoni.
Mnamo 2020, alijitetea dhidi ya wakosoaji kwenye video ya YouTube iliyoitwa “not my responsibility” alipoonekana akicheza kama wanawake wa “madanguro” (stripping).
Sihitaji yeyote kufahamu chochote kuhusu mimi ndiyo sababu ninavaa nguo kubwa sasa.
Hakuna mtu anayeweza kuwa na maoni kwa sababu hawajaona kilicho ndani yangu au chini ya mambo.