Wakati dunia leo ikiadhimisha siku ya usafi wa masikio wataalamu wa afya wamesema kitendo cha mtu kuchokonoa sikio kwa ajili ya kulisafisha ni kinyume na utaratibu ambao mwili wa binadamu umejiwekea ili kusafisha kiungo hicho cha mwili.
Watalamu wamesema kitendo cha kuchokonoa kwa kutumia kalamu, pamba, kijiti inaweza kuleta madhara makubwa kwa afya.
Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa sikio limegawanyika katika sehemu kuu tatu ambapo kuna sehemu ya nje, kuna sehemu ya katikati na sehemu ya ndani kwa hiyo kila sehemu ufanya kazi yake na kila sehemu upaswa kufanyiwa usafi maalumu.
Sehemu ya nje ndiyo ambayo ukusanya mawimbi ya sauti kwa hiyo tunapaswa kusafisha sehemu hiyo kwa kutumia kitambaa na maji safi na kuhakikisha hiyo sehemu haina vidonda hata kimoja kwa hiyo kila siku tunapopooga tunapaswa kufanyia sehemu hii usafi wa kutosha.
Sehemu nyingine ni sehemu ya katikati hii ni sehemu ambayo upokea mawimbi ya sauti na kuyabadilisha yakawa kwenye sauti fulani ambayo baadaye usafilishwa , sehemu hii uwa na wax ambazo uzaliwa kwenye sikio kwa hiyo uweza kutolewa na Pamba na tuepuke kuweka vitu vyenye ncha kali kwenye sehemu hii.
Sehemu ya tatu ya sikio uitwao sehemu ya ndani ambayo kazi yake ni kusafilisha mawimbi ya sauti na kuyapeleka ili yaweze kutafsiriwa na mtu uweza kusikia na kitendo hiki utumia mda mfupi sana katika sehemu hii huwa kuna uchafu kwa hiyo tunaangalia kwa kutumia tochi na uchafu ukigundulika utolewa kwa kifaa maalum cha kusafishia sikio kwa hivyo hatupaswi kutumia vijiti kutolea uchafu sehemu hii mpaka kifaa maalum.