Chama cha kisiasa cha Kikristo chakata rufaa, kikisema kuwa ni kinyume cha demokrasia kuuza na kununua pombe hivyo liwekwe katazo mara moja.
Unywaji wa pombe hadharani hauruhusiwi nchini Iraq, nchi yenye Waislamu wengi, lakini inaweza kununuliwa katika maduka ya vileo au baa zilizo na leseni.
Sheria hiyo, iliyopitishwa awali na bunge mwaka 2016, inatoza faini ya hadi dinari milioni 25 za Iraq (£14,256).
Sheria hiyo inakataza uuzaji, uagizaji au utengenezaji wa pombe na ikawa rasmi tu mwezi uliopita, miaka saba tangu kupitishwa, baada ya kuonekana kwenye gazeti rasmi la serikali.
Bado haijulikani ni kwa kiasi gani sheria inaweza kutekelezwa, na ikiwa Mahakama ya Juu ya Shirikisho itaiondoa sheria hiyo.
Sarmad Abbas, wakala wa majengo mji mkuu wa Iraq Baghdad, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba marufuku hiyo ingesukuma tu uuzaji wa pombe kwenye soko la biashara.
Alikiri kwamba mafundisho ya Waislamu yanakataza unywaji wa pombe.
“Lakini hiyo ni uhuru wa mtu binafsi ambao huwezi kuwakataza wananchi kuufanyia kazi,” alisema.