Iwao Hakamada, mfungwa ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 87, ndiye mfungwa aliyefungwa aliyeishi gerezani kwa muda mrefu zaidi huku akisubiri hukumu ya kifo, kulingana na shirika la haki za binadamu la kimataifa la Amnesty International.
Alihukumiwa kifo mwaka 1968 kwa maujai ya bosi wake, mke wa mwanaume huyo na waoto wao wawili katika mwaka 1966.
Mwanamasumbwi huyo wa zamani wa ndondi za kulipwa alikiri mauaji hayo baada kuhojiwa kwa siku 20 ambapo alisema alipigwa. Baadaye aliondoa ushahidi wake wa kukiri kosa mahakamani.
Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamekosoa utegemezi wa Japan kuhusu kukirimakosa, ambapo walisema polisi hutumia nguvu mara kwa mara kuwalazimisha washukiwa kukiri mashitaka.
Iwao Hakamada alikamatwa na kushutumiwa kwa wizi na mauaji ya muajiri wake na familia yake katika kiwanda cha kusindika soya kilichopo Shizuoka magharibi mwa jiji la Tokyo mwaka 1966 na walipatikana wakiwa wamekufa kwa kuchomwa kisu.
Katika kesi mpya, majaji watataka kubaini iwapo vinasaba DNA kutoka kwenye madoa ya damu iliyopatikana kwenye nguo inayodai wa kuvaliwa na muuaji vinafanana na na vya Bw Hakamada.
Hakamada, ambaye amekuwa nje kwa kuachiliwa kwa muda tangu 2014 kwa misingi ya kibinadamu, awali alikanusha madai hayo lakini baadaye alikiri, na kisha kudai kwamba polisi walikuwa wamemtisha na kumshambulia wakati wa siku 20 za mahojiano.