Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa mradi wa maji wa Mwanga, Same hadi Korogwe utakamilika kwa kipindi cha miezi kumi na nne na sio kumi na nane kama Mkandarasi alivyo omba kwani Wananchi wana uhitaji mkubwa wa huduma ya maji safi na salama.
Akizungumza wakati alipotembelea mraadi huo na kuzungumza na Wananchi wa Same, Waziri aweso amesema kuwa Wananchi wa Same na Mwanga wamevumilia sana kupata majisafi na salama kwa kipindi kirefu hivyo ni wakati sahihi sasa mradi huo kuanza utekelezaji wake kwani Serikali inayoongozwa na Rais Samia imedhamiria kumaliza miradi yote ya maji ambayo ilikwama kwa kipindi kirefu.
“Mlisema mnaweza kukamilisha mradi huu kwa miezi kumi na nane na sisi kama Wizara tukasema hapana Wananchi hawa wameshasubiri maji kwa kipindi kirefu sana na nitumie nafasi hii kuwaomba radhi sana Wazazi wangu”
Mradi huo wa maji ambao unatarajiwa kugharimu shilingi 262 bilioni utawanufaisha zaidi ya Wananchi 438,000 ambapo Wizara imeuwisha mkataba wa utekelezaji wa mradi huo kwa Mkandarasi BADR EAST AFRICAN ENTERPRISES LTD.