Nigeria sasa itafanya sensa yake ya kwanza katika kipindi cha miaka 17 mwezi Mei badala ya mwisho wa Machi waziri wa habari alisema Jumatano, akitaja kupangwa upya kwa uchaguzi wa ugavana kwa uchelewesho huo.
Sensa katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika inapelekea kusahihisha taarifa kuhusu idadi kamili ya watu na ukubwa wa makabila tofauti.
Waziri wa Habari na Utamaduni Lai Mohammed aliwaambia wanahabari kwamba kucheleweshwa kwa uchaguzi wa magavana wapya kwa wiki moja hadi Machi 18 kunamaanisha kuwa kulikuwa na muda mchache wa kuandaa hesabu ya watu.
Idadi ya watu nchini Nigeria inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 200 na Umoja wa Mataifa unatarajia idadi hiyo kuongezaka maradufu ifikapo mwaka 2050.
Hilo litafanya Nigeria kuwa nchi ya tatu kwa kuwa na watu wengi duniani nyuma ya China na India kuipiku Marekani.
Mohammed hakusema ni lini mwezi wa Mei sensa hiyo itafanyika tangu kufanyika kwake mwaka 2006.