Uwanja huu umefunguliwa kongamano la FIFA la 73 linalowajumuisha wajumbe 2,000, likitarajiwa kuanza rasmi hii leo mjini Kigali.
katika kongamano hili ambapo uchaguzi wa FIFA utafanyika Rais wa sasa wa FIFA Infantino ndiyo mgombea pekee wa kiti hicho baada ya kutokuwa na mpinzani.
Baada ya uzinduzi wa Uwanja wa Pele wa Kigali washiriki wa Kongamano hilo walicheza mechi ya soka, timu moja ikiongozwa na Rais wa Rwanda Paul kagame huku timu nyingine ikiongozwa na Rais wa FIFAGianni Infantino.
Rais Kagame ambaye anafahamika kama shabiki wa mpira wa migu hususan wa timu ya Uingereza ya Arsenal – ambaye hucheza mchezo wa tenesi, aliwashangaza wengi alipojitokeza uwanjani kucheza soka.
Mwezi January, wakati wa mazishi ya Pele,Infantino, ambaye anamuelezea Pele kama mwanamichezo wa mfano wa kuigwa alliahidi kuiomba kila nchi duniani kuupatia jina la Pelé uwanja, kwa heshima ya Mchezaji bora wa Brazil na dunia.
Rwanda, ambayo inapokea kongamano la 73 la FIFA ni miongoni mwa nchi ambazo zimetekeleza ombi hilo.