Usiku huu kutoka Ukumbi wa Mlimani City, Clouds Media Group imeandaa KONGAMANO lililohusu Wizara ya Maji kama sehemu ya Event yao ya kurasa 365 volume II yenye lengo la kuangazia yaliyofanyika katikasekta Ya Maji Kwenye Kipindi Cha Miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika shughuli hiyo ambayo imeenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa, Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye alipata nafasi ya kuzungumza na kuelezea walipotoka kama Wizara, changamoto walizozipitia na hata mafanikio waliyoyapata Kwa kipindi Cha miaka miwili.
“Wizara tulipotoka ilikuwa Wizara ya kero na lawama niliwahi kwenda Mbeya Vijilini eneo linaitwa Garijembe badala ya kupelekwa eneo la Mradi wa Maji mtaalamu anakuzungusha ila hela zilitolewa na hakuna kilichofanyika”- Waziri wa Maji Jumaa Aweso
Nilipofika eneo ambalo Mradi ulitakiwa kuwepo nilikuta hakuna mradi wowote. Tulimuita mkandarasi tukamuuliza vipi mbona hakuna kilichofanyika akajibu Nimegawana hela na mtaalamu zikitolewa Milioni 30 zake milioni 15 zangu milioni 15 nilishangaa”- Waziri wa Maji Jumaa Aweso
“Niliwahi kufuatilia Mradi kwenye eneo moja linaitwa Mwakitolio Shinyanga huko. Nilipofika pale nikauliza Mradi ulipo naona mtaalamu anasema Mheshimiwa naomba nikunong’oneze nikamwambia hapana sema mbele ya Wananchi wakusikie akaniambia Mheshimiwa hakuna eneo lina wachawi kama hili, usiku mabomba yanapaa”
“Wakati mwingine tatizo ni mtazamo tulikuwa na miradi ya maji 177 huko Bwire. Tayari Miradi 157 imekamilika na miradi ilivobaki tunatarajia kuimaliza mwaka huu.
Zilitoka fedha za Uviko na katika Wizara yetu Rais alitupa Tsh bilioni 135. Kupitia fedha hizo tumejenga miradi 174 vijijini na mini tumejenga miradi 44 jumla ni miradi 218 kwa fedha alizotoa Rais wetu.” Waziri Aweso