Mtoto wa kiume wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni Muhoozi Kainerugaba anasema yuko tayari kujenga sanamu ya marehemu mwimbaji wa Marekani Tupac katika mji alikozaliwa huko Marekani, iwapo watu wa taifa hilo wameshindwa kufanya hivyo, Zaidi ya miaka 25 tangu kifo chake.
Muhoozi ambaye hivi majuzi alitangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa 2026, alipendekeza kuwa anataka kusaidia Wamarekani kwa kujenga sanamu ya mwanamuziki huyo maarufu.
Mwanamuziki huyo Tupac Amaru Shakur lakini maarufu akifahamika kwa jina la kisanii la 2Pac, ni miongoni mwa wasanii maarufu wa wakati wote ambao wameuza zaidi ya rekodi milioni 75 duniani kote.
Muhoozi alitweet akisema “Ikiwa ndugu na dada zetu wapendwa huko USA hawajajenga sanamu kubwa ya mwimbaji mkuu wa Kiafrika wa kizazi chetu, nataka kusaidia. Nataka kujenga sanamu ya Tupac katika mji wake alikozaliwa. Mzee apumzike kwa amani!”
“Nataka kujenga sanamu ya Tupac katika mji wake alikozaliwa apumzike kwa amani!”
Alizaliwa mwaka wa 1971, 2Pac amebakia rapa bora duniani hata katika kifo chake, katika kazi yake ya filamu na muziki.
Mwanamuziki huyo alifunga ndoa na mpenzi wake wa wakati huo Keisha Morris, mwanafunzi wa sheria ya awali mwaka wa 1995, lakini ndoa yao ilibatilishwa miezi kumi baadaye.
Hata baada ya kifo chake, 2Pac ametunukiwa na kusherehekewa kutokana na mchango wake katika tasnia ya muziki na filamu