Mkuu wa Wilaya ya Mlele mkoani Katavi Alhaj Mjid mwanga amesema Tangu Rais wa awamu ya sita Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan aingie madarakani ametoa zaidi ya Bilioni Mia moja (196.6)Kwa wilaya hiyo katika miradi ya maendeleo ikiwemo, Miundombinu ya Afya,Elimu,Maji , Barabara na umeme.
DC Majid ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa Wilaya hiyo katika hafla maalum ya iliyoandaliwa yenye lengo la kueleza mambo mbalimbali yaliyotekelezwa na serikali ya awamu ya sita kwa miaka miwili.
Majid Anasema kuna Kila haja ya wananchi kumshukuru Rais Samia Kwa makubwa aliyofanya ambapo amewataka kutunza miundombinu yote inayojengwa kama baraba, maji na umeme. Kwani ni muda mfupi tu ujao Wilaya itaanza kutumia umeme wa Grid ya Taifa kutokea Tabora hivyo nilazima tuitunze kwa gharama kubwa.
Kwa upande wa mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya Mbimbwe Bi. Catherine Mashalla na Kaimu mkurugenzi halmahauri ya Mlele Bwana Luke Kifyasi wamesema kupatikana Kwa fedha Hizo kumeleta maendeleo makubwa sanaa katika Halamashauri zao na kuwezesha huduma kupatikana kwa urahisi kwa wananchi.