Wakati Aprili 13, ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Kampuni ya Repatriation kwa Kushirikiana na Clouds Media Group wameandaa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya uandaaji wa makala ya Mwalimu Nyerere.
Akizungumzia mchakato huo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dr.Jakaya Kikwete, Mkurugenzi Mtendaji wa Repatriation amesema…”Tumeandaa Fund Rising Dinner, nia na madhumuni ya kuandaa ni kwa ajili ya kutengeneza global documentary ama kwa Kiswahili ni kumbukumbu ama Makala ya maisha ya Mwalimu Nyerere na tutatembea nchi zaidi ya 15″
“kwa ajili ya kukusanya taarifa za Mwalimu kwa sababu alisaidia nchi nyingi za Afrika kupigania uhuru na tunataka kumbukumbu ibaki kwa kizazi cha sasa na baadaye, mgeni rasmi tunatarajia atakuwa Rais Mstaafu Kikwete, hivyo wito mkubwa tunatoa kwa taasisi na Kampuni tushirikiane ili tufanye jambo hili kwa sababu la watu wote,”.amesema