Mfanyabiashara Maarufu Jijini Arusha,Richard Poul maarufu kwa jina la Marcas amajitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi Moja ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu{NEC} Mkoa wa Arusha akisema kuwa lengo lake kuu ni kuwaunganisha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} kuwa kitu kimoja na ili kiweze kuendelea kushika dola.
Marca alisema na kuwataka wajumbe wa Uchaguzi kuangalia sifa za mgombea na kuacha mara moja kuchagua mgombea kwa rushwa kwani rushwa kwake ni adui wa haki na kamwe hawezi kufanya hivyo kwani anajiamini kuwa anatosha.
Amesema kuwa uchaguzi huo wa marudio uligubikwa na rushwa na ndio maana viongozi wa juu wa CCM Tiafa waliufuta kw amaslahi ya chama hivyo basi wajumbe wa Uchaguzi wasirudie tena makosa hayo kwani ni kuendelea kukidhallisha chama kwa tama za watu wachache.
Uchaguzi huo ambao ulikuwa ufanyike Novemba mwaka jana ulifutwa kutokana na vitendo vya rushwa.