Mkuu wa Wilaya ya hanang Mkoani Manyara Janeth Mayanja, amewataka wakulima Wilayani humo kuacha tabia ya kuchukua mikopo bila kuweka malengo nakuwasihi kulima kilimo cha kisasa ili kunufaika na kilimo hicho pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mayanja amesema hayo katika maonesho ya zana za kilimo yaliyoandaliwa na kampuni ya Agricom Africa, ambao wamekuwa wakiwawezesha wakulima kulima kilimo cha kisasa kwa kutumia zana za kisasa na kuongeza kipato.
Baadhi ya wakulima wamesema walikuwa wakipita changamoto za ukosefu wa Mashine katika kuhakikisha wanalima kilimo cha kisasa ila kwasasa uwepo wa Mashine hizo unakwenda kamsaidia mkulima kuongeza kipato pamoja kukuza uchumi kwa wakulima na kusaidia kupunguza muda mrefu ambao walikuwa wakiutumia shambani kwa mkono.
Kwa upande wake Peter Temu meneja wa Agricom Kanda ya kati amesema baadhi ya wakulima wakuwa wakishindwa kumudu gharama za zana za kilimo lakini kupitia wadau na taasisi za fedha wanawawezesha kupata elimu pamoja na mikopo iliyonafuu ili kuwawezesha kupata zana Bora za kilimo.