Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza limefanya misa takatifu ya kumuombea Hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano.
Misa imefanyika kwenye viwanja vya madhabahu ya Bikra Maria, Kawekamo Mwanza na kuhudhuliwa na Viongozi akiwemo Spika Mstaafu Anne Makinda, Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina pamoja na Prof. Costa Ricky Mahalu Makamu Mkuu wa Chuo cha SAUTI Mwanza.
Mhashamu Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza Lenatus Nkwande ameeleza kuwa wakati tukiendelea kumuombea mpendwa wetu vi vyema kukumbuka yote aliyoyahimiza enzi ya uhai wake, uzalendo wa kweli, kudumisha amani, undugu pamoja na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Ameongeza kwa kuitaka jamii kukemea vikali mahusiano ya jinsia moja kwani sio tamaduni za Kitanzania na kuwahusia Viongozi wa siasa ambao wanamzungumzia Hayati Magufuli kwa mambo mabaya waache kwani sio jambo zuri kumhusisha mtu alietangulia mbele za Haki.
Mwakilishi wa familia ya Hayati Magufuli Ngusa Samike ametoa shukrani za familia kwa Watanzania kwa kuendelea kumkumbuka mpendwa wao ikiwa ni miaka miwili sasa tangu kuondokewa na mpendwa wao.
Hayati Dkt. John Magufuli march 17, 2023 ametimiza miaka miwili tangu afariki akiwa madarakani usiku wa march 17, 2021.