Mbunge wa Jimbo la ‘Hanang’ Mhandisi Samwel Hhayuma amesema uwepo wa Baraza la Ardhi Wilayani Hanang’ itasaidia kupunguza migogoro ya Wakulima na Wafugaji pamoja na kuondoa gharama kwa Wananchi waliokuwa wakilazimika kusafiri kufuata huduma Wilaya ya Babati.
Hhayuma amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ardhi Wilayani humo huku akipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa Wananchi wake.
“Nifuraha Sana kwangu kuona kile nilichokipigania Bungeni kimetekelezwa na Serikali yangu ya Chama Cha Cha Mapinduzi ,nilitaka kushika shilingi kwenye Bajeti ya 21/22 na Waziri aliahidi kujengwa Baraza Hanang’ na leo hii imejengwa hii inayoshesha kuwa Serikali ikiahidi inatekeleza, sauti ya Wabunge inasikilizwa”
Amesema Hanang’ ina ardhi yenye rutuba kila ambapo kila mtu anahitaji kipande cha ardhi ili azalishe mali hivyo uwepo wa Baraza hilo utasaidia katika utambuzi na umiliki halali wa ardhi na kutambulika kisheria.