Katibu tawala msaidizi mkoa wa Morogoro Herman Tesha amewataka viongozi wanaohusika na mfumo mshitiri wa vifaa tiba, dawa na vitendanishi katika halmashauri za Wilaya kuhakikisha wanasimamia vema mnyororo mzima wa uagizaji hadi kumfikia mgonjwa na hivyo kudhibiti upotevu wa dawa.
Akifungua mafunzo ya Mfumo mpya utakaokua unafanyika kwa njia ya kielecktroniki kwa Maafisa wa Halmashauri tisa za Mkoa huu, Tesha amesema kumekuwepo na malalamiko mengi ya Ukosefu wa Dawa kwa Wagonjwa.
Tesha anasema licha ya Serikali kuleta dawa kwenye Vituo vya Afya Zahanati na hospitali bado kumekuwa na changamoto ya upatikanaji huduma za matibabu hivyo lazima Maafisa wote washiriki katika upokeaji na utoaji dawa.
“Malalamiko ya ukosefu wa dawa yamekua mengi Kwa Wagonjwa hivyo serikali inatoa dawa Lakini zimekua zikitumika kinyume na Matumizi yaliyopangwa Hilo Jambo lazima tulikomeshe”
Kwa upande wake Dkt Abilah Njopeka ni muwezeshaji wa kitaifa na FIONA CHILUNDA ni mshauri mwandamizi wa mfumo huo kupitia mradi wa kuimarisha afya wa HPSS ambao ndio wafadhili wa mfumo huo wamesema mfumo huo mpya utasaidia Kuthibiti Changamoto hiyo.
Nao baadhi ya Wananchi mkoani Morogoro wameishukuru serikali kwa kutafuta Njia za Kuthibiti mianya ya upotevu dawa hivyo wanaamini huduma itaimarika sehemu za kutolea huduma za afya
“Unaenda hospitali unaambiwa dawa amna unaelekezwa ukanunue Duka fulani hii inatupa Mashaka naipongeza Serikali kwa uamuzi huu utasaida”