Muungano wa makampuni ya kimataifa, yakiwemo Google na Microsoft, Jumatano yameushutumu mswaada uliopitishwa na bunge la Uganda wiki iliyopita dhidi ya ushoga na kuionya kuwa sheria hiyo itakuwa na athari za kiuchumi kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Ikulu ya White House wiki iliyopita ilipitisha mswaada ambao unatia wasi wasi na kwamba ni miongoni mwa hatua kali sana zilizochukuliwa dhidi ya jumuiya ya mashoga duniani.
Mswaada wa sheria hiyo unaweka adhabu ya kifo kwa wale watakao tenda vitendo vya ushoga uliokithiri.
mswaada huo pia umefafanua kuwajumuisha wale watakao jihusisha na mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja na watoto wenye umri chini ya miaka 18 au wakati mhusika ana Virusi Vya Ukimwi, miongoni mwa makundi mengine.
Museveni bado hajatoa maoni yake kuhusiana na mswaada huo, ingawa aliwahi kutia saini sheria kama hiyo mwaka 2014 ambayo ilizua tuhuma za kimataifa kabla ya kubatilishwa na mahakama ya ndani ikidai sheria hiyo haikufuata taratibu za kimsingi.