Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan imezidi kufungua fursa kwa wawekezaji ndani na nje ya nchi katika sekta ya madini kwa kuweka mazingira rafiki Zaidi kufanya biashara.
Kampuni ya Aria International commodies Limited pamoja na BECCO leo imefanikiwa kusafirisha Zaidi ya tani elfu 50, huku wakiwa na matarajio ya kusafirisha Zaidi ya tani laki 1 kwenda masoko ya nchi za nje Asia, Ulaya na nchi nyingine za Afrika.
Hayo yamesemwa na Meneja wa uendeshaji wa Kampuni ya Aria Commodities International Limited, Ndg. Lazaro William Kandore.
Kwenye upande wa uzalishaji wa makaa ya mawe mpaka sasa Aria International kwa kushirikiana na BECCO inafanya shughuli za uchimbaji kwenye migodi ambayo ipo Ruvuma, Mbinga , Songea iliyokwisha zalisha Zaidi ya tani 450,000 na kutoa fursa za ajira kwa watanzania Zaidi ya 400.
Akizungumza na wana Habari Bw, Lazaro amesema Kampuni zao zinapenda kumshukuru sana Mhe, Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira Rafiki Zaidi kwa viwanda na migodi ya makaa ya mawe kwani imechangia ongezeko la uzalishaji Pamoja na ukuaji wa biashara hii katika nchi ya Tanzania.