Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini upande wa Tanzania Bara na Zanzibar wameshuhudia maboresho ya miundombinu, mifumo na manunuzi ya vifaaa vya kisasa katika bandari ya Dar Es Salaam yaliyochangia ongezeko la Meli, shehena na mapato ya Serikali.
Maafisa hao wakiongozwa na mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari Maelezi Zamaradi Kawawa wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa Bandarini ulioleta mageuzi ya kiufanisi.