Rais Paul Kagame alichaguliwa tena kwa muhula wa miaka mitano kama kiongozi wa cha tawala cha Rwandan Patriotic Front, RPF) kwa wingi wa kura, sawa na 99.8% ya kura.
Mkuu wa nchi na mwanachama mwanzilishi wa chama hicho alikosa kura tatu ili aweze kuchaguliwa kwa kauli moja, huku mgombea mwingine mmoja tu akishindana naye, Abdul Karim Harerimana, mbunge wa zamani na ambaye aliteuliwa kuwa balozi wa Rwanda nchini Indonesia mwishoni mwa Machi.
Makamishna 25 na wengine wa kamati kuu walichaguliwa Jumapili. Seneta wa zamani Consolée Uwimana anakuwa makamu wa rais wa RPF, mwanamke wa kwanza kushika nafasi hii katika chama hiki tawala.
Anachukua nafasi ya Christophe Bazivamo katika wadhifa huo tangu mwaka 2002.
Balozi wa Rwanda nchini Angola, Wellars Gasamagera, anachukua nafasi ya katibu mkuu wa chama.
Kongamano la 35 la chama cha rais nchini Rwanda, Rwandan Patriotic Front, ulifanyika wikendi hii huku zaidi ya wajumbe 2,000 wakipiga kura siku ya Jumapili kwa kamati mpya ya utendaji ya chama chao, na bila ya kushangaza wakamchagua tena Rais Paul Kagame kama kiongozi wa chama
Kamati mpya ya utendaji ya RPF itakuwa na jukumu hasa la kutayarisha chama kwa ajili ya uchaguzi huo.
Mkuu wa nchi kwa miaka 23, Paul Kagame, bado hajazungumza kwa uhakika kuhusu uwezekano wa kugombea muhula mpya wa urais.