Marla McEntire bila kujua alimbeba mtoto wake hadi wiki ya 40, ingawa alikuwa kwenye udhibiti wa uangalizi wa daktari alisema alipima ujauzito, na matokeo yake yalikuwa hasi, hivyo basi kudhani kwamba hakutarajia kujifungua.
Hata hivyo, alipokuwa chooni mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34 alianza kupata uchungu wa kuzaa lakini akadhani ni kuvimbiwa, kama ilivyoripotiwa na Daily Mail.
‘Nina umri wa miaka 34, sijawahi kuwa na hofu ya ujauzito hapo awali nlipata ujauzito Mei na sikuwahi kuonyesha, yaani tumbo langu halikuonesha mabadiliko na kuwa kubwa,sikuwahi kupata morning sickness, sikuwahi kuhisi hata kizunguzungu na kufikiabJanuari, nilianza kuwa na maumivu ya nyonga na matatizo ya tumbo kwa hivyo nilienda kwa daktari na hakuna aliyegundua kuwa kulikuwa na mtoto mle ndani,’ alieleza wafuasi wake kwenye TikTok’.
“Kwa hivyo nilikuwa najisaidia kwenye choo, nilitazama chini na kuona kiumbe kama mtotot kwamba yuko hai na nikampigia kelele baba yangu na alikuja pale na kunisaidia kumtoa mtoto kwenye choo kwa sababu ni wazi bado ilikuwa kazi ngumu kwangu kumtoa nje’.
Kwa hivyo Babake Marla aliwasiliana na 911 na wakamwelekeza jinsi ya kukata kitovu ingawa alisema hakuridhika na wazo hilo:
Marla na mwanza aliyemwita Atlas walisafirishwa hadi hospitali ya eneo hilo na inasemekana wanaendelea vizuri lakini alisema kwa sasa ana fuatilia kuhusu baba wa baba wa Atlas.
Atlas alizaliwa mnamo Februari 27, na mama huyo mpya anasema anashukuru kwa familia yake na marafiki ambao walinunua vitu muhimu vya mtoto dakika ya mwisho.