Jeshi la Polisi Mkoani Tanga linamshikilia Hassan Nyundo (25) Mkazi wa Kijiji cha Vue kata ya Mowa Wilayani Mkinga kwa tuhuma za kumchoma kisu Amiri Mohamed (30) huku ikidaiwa kwamba sababu mojawapo ya ugomvi ni kitendo cha Amiri kumuomba maji ya kunywa wakati akifahamu kuwa Hassan amefunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Akiongea na @ayotv_, RPC wa Tanga Henry Mwaibambe amesema kuwa 05/04/2023 majira ya saa sita mchana Amiri na Mtuhumiwa walikuwa wakiishi nyumba moja hivyo hadi mauti yanamkuta Amiri alimshinikiza Mtuhumiwa kumpatia maji ya kunywa kitendo kilichomchukiza Hassan (Mtuhumiwa) na kusababisha ugomvi uliopolekea kumchoma kisu kulikosababisha kufia njiani wakati kiwaishwa Hospitali.
Kamanda Mwaibambe amesema hadi sasa kuna taarifa mbili juu ya tukio hilo ambapo wengine wanasema Mtuhumiwa alichukizwa na kitendo cha Amiri kumuomba maji pamoja na kunywa maji wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani lakini wengine wanasema ni ugomvi wa kawaida.
“Kwakweli hadi sasa chanzo kamili cha tukio hilo bado hakijajulikana kwani hawa wawili ni ndugu waliokuwa wakiishi nyumba moja, ni mauaji ya kusikitisha sana haiwezekani ugomvi wa maji tu unachomoa kisu una mchoma mwenzako, kwakweli huu ni mmomonyoko mkubwa wa maadili”