Watu sita wamehukumiwa kifungo cha maisha jela huko Kinshasa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya balozi wa Italia, mlinzi wake na dereva mnamo Februari 2021, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Kijeshi ya Jamhuri ya Kidemnokrasia ya Congo.
Licha ya kuwa, adhabu ya kifo ilikuwa imeombwa na mwendesha mashtaka wa umma, lakini haikuzingatiwa na mahakama ya kijeshi ya Kinshasa-Gombe, ambayo imetoa uamuzi wake.
Upande wa utetezi umeziambia duru za habari kwamba utakata rufaa. Kwa hiyo kesi nyingine itasikilizwa mbele ya mahakama ya kijeshi.
Wafungwa wa tano kati ya sita wanazuiliwa katika jela la kijeshi la Ndolo, na wa sita yuko mafichoni.
Watu hao walishtakiwa kwa mauaji, kushirikiana na kundi la wahalifu, kumiliki silaha kinyume cha sheria na risasi za vitu ,walipatikana na hatia ya mauaji mnamo Februari 22, 2021 ya balozi wa Italia katika Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo, Luca Attanasio, mlinzi wake Vittorio Iacovacci, na dereva wa shirka la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) nchini DRC, Mustapha Milambo.