Kisa hicho kilitokea katika Shule ya sekondari ya Lamar, ambapo picha zinaonyesha mwanafunzi huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 15 akizozana na mwalimu ambaye inasemekana alichukua simu yao ya mkononi.
Sekunde chache baadaye, mwanafunzi alimpiga mwalimu ngumi usoni huku mashahidi wakishangazwa na shambulio hilo na kupiga yowe huku mwanafunzi huyo akiendelea kurusha ngumi zaidi, na video hiyo ilikatwa.
Rais wa Shirikisho la Walimu wa Texas Marekani Zeph Capo alisema katika taarifa yake kwamba mwanafunzi huyo hapaswi kuruhusiwa kurudi shule kwani tabia yake haipaswi kuvumiliwa.
“Kwa vyovyote vile, hatakiwi kuruhusiwa kurudi shuleni kwani hilo si jambo linalohitaji kuvumiliwa. Kwa bahati mbaya, tunaona mengi kama haya,” Capo alisema. “Tunaona mengi ya haya yakifanyika kwa walimu wetu na kwa wafanyikazi wetu wa shule,” alisema
Chama hicho pia kiliwahi kuripoti tukio kama hilo kwani katika mwaka wa shule wa 2021-2022, kulikuwa na matukio 520 yanayohusiana na shambulio dhidi ya wafanyikazi.
Capo alisema ana uzoefu wa wanafunzi kurusha madawati na nyakati ambapo baadhi ya wanafunzi walionyesha tu hasira darasani.
Hata hivyo, anasema hajawahi kushambuliwa katika shule yeyote.
Ujumbe ulitumwa nyumbani kwa wazazi kuhusu tukio hilo ikisema ;tabia hiyo haitavumiliwa kwani wasimamizi wanaangalia mikakati ya kuzuia visa zaidi katika siku zijazo kwa wanafunzi wala walimu alitoa maoni yake kuhusu tukio hilo.