Anaitwa rona mjasiriamali anayetengeneza sabuni na products za ngozi ikiwemo mafuta, scrab na vitu vingine kwa zaidi ya miaka 10 alijitafuta na kujipata mama mwenye watoto watatu aliyeanzia ujasiriamali jikoni kwake kwa kutumia sukari na mchele kutengeneza bidhaa za kuipendezesha ngozi ya mwadamu.
Rona alianza miaka zaidi ya 10 iliyopita akijifanyia nyumbani kwake tena jikoni akiamini siku moja atakua mfanya biashara mkubwa na bora kuliko wengine.
kiu yake ilikuwa kwenye kufanya maajabu ambayo huenda wengine hawajayaona kwenye nyanja ya urembo , kufanya makubwa na ndio maana hakusita kwenda shule kujisomea na kupitia sido akaamua kujisajili na hivi sasa na yeye anamiliki kiwanda chake kidogo cha utengenezaji wa product zake natural ni dada wa kichaga aliyetumwa pesa na akajua kuitafuta haswaaa lakini pia ametoa ajira kwa watu wengine wasio pungua kumi.
Hakuamini kwenye kuajiriwa na ndiomana leo kaajiri wengine na anajivunia hilo.”Haijalishi safari yako utaianza vipi lakini la msingi ni utakavyoimaliza”.
Hana makuu wala majivuno na ndiomana leo ayo tv inamsogeza kwako ukamjue na kujifunza jambo kutoka kwa mkali huyu
PLAY hapa chini kutazama Full Interview