Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, mafuriko ya ghafla na kufurika kwa mito kunakotokana na mvua kubwa nchini Somalia kunaweza kusababisha milipuko ya magonjwa yanayotokana na maji kwani mvua hizo zimekuja wakati mlipuko wa kipindupindu na kuhara umeripotiwa katika mkoa wa Jubaland, kusini mwa Somalia, na mkoa wa Kusini Magharibi.
Ikinukuu takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya ya Somalia, OCHA imesema karibu kesi 4000 zinazoshukiwa kuwa na kipindupindu na vifo 17 vinavyohusishwa na ugonjwa huo vimeripotiwa katika wilaya 27 nchini humo tangu mwezi Januari na imesema, maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko ni wilaya ya Bardhere mkoani Gedo, kusini mwa Somalia, na wilaya ya Baidoa iliyoko mkoa wa Bay, kusini magharibi mwa Somalia.
Msimu wa Gu (mvua) kawaida huanzia Aprili hadi Juni na Ikiwa mvua kubwa itaendelea kunyesha nchini Somalia na katika nyanda za juu za Ethiopia katika msimu huu, washirika wanakadiria kuwa mafuriko ya ghafla na ya mito yanaweza kuathiri hadi watu milioni 1.6, na zaidi ya 600,000 wamekimbia makazi,” OCHA ilionya.
Ilisema kuwa watu wengi waliokimbia makazi yao wangetokea katika maeneo yenye mito kando ya mito ya Juba na Shabelle, na sehemu za mikoa ya Bay na Banadir yenye mafuriko ya ndani huko Galmudug, Puntland na Somaliland.
OCHA ilisema zaidi ya watu 21 walikufa kutokana na mafuriko katika wilaya ya Bardhere, Jimbo la Jubaland, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kuanzia Machi 21 hadi 24 na mvua hizo kubwa na mafuriko yamekuja kufuatia misimu mitano ya ukame ambayo imesababisha zaidi ya Wasomali milioni 1.4 na kuua mifugo milioni 3.8 tangu katikati ya 2021, shirika la Umoja wa Mataifa lilisema.