Maafisa wa usalama na forodha walikamata bangi hiyo katika bandari ya kaskazini ya Tangier ikiwa ndani ya lori la kimataifa la mizigo, Kurugenzi Kuu ya Usalama wa Taifa (DGSN) ilisema Jumamosi jioni
Polisi wa Morocco walikamata tani 5.4 za bangi zilizokuwa zimefichwa ndani ya lori lililokuwa likielekea Uhispania na kilo 60 za cocaine zilizojazwa kwenye samaki aina ya Tuna waliogandishwa barafu, maafisa wa usalama wamesema.
Maafisa wa usalama na forodha walikamata bangi hiyo katika bandari ya kaskazini ya Tangier, ikiwa ndani ya lori la kimataifa la mizigo, Kurugenzi Kuu ya Usalama wa Taifa (DGSN) ilisema Jumamosi jioni.
Paketi hizo zilichomekwa kwenye fito nyembamba zilizopangwa kwenye upenyo maalum ndani ya gari. Dereva huyo raia wa Morocco mwenye umri wa miaka 45 alikamatwa.
Katika operesheni tofauti pia huko Tangier karibu kilo 60 za cocaine zilikamatwa Alhamisi ndani ya kontena lenye jokofu, polisi walisema. Cocaine ilijazwa kwenye makopo ya tuna ikiwekwa alama kama inatoka Ecuador na kuelekea Uhispania.