Chuo Kikuu cha Dar es saalam kimewaomba Watanzania wanaokosoa prototype ya gari (Golf Car) waliyoitengeneza kuwa Wazalendo na kupenda vya nyumbani kwa kuwatia moyo lakini pia wasiishie kukosoa tu bali washauri vitu gani vifanyike ili kuboresha ubunifu huo.
Mtaalamu wa umeme Mhandisi Anthony Nyenyembe ambaye ni miongoni mwa Timu ya zaidi ya Watu kumi waliotumia miezi mitatu kutengeneza prototype ambao anasema baada ya kufanikiwa kuifanya itembee sasa wataanza rasmi kutengeneza magari halisi kama Nchi nyingine na kwa kuanzia wamepewa oda ya Geita Gold Mining (GGM) kutengeneza gari la Polisi na Ambulance.
“Shida hapa sio Body ya gari wala taa wala nini na gari ni engine, shida ni jinsi gani engineering na utafiti wetu umetumika kufanya gari hili kwa kutumia umeme wa Tsh.Elfu moja au Elfu 3 likatembea KM 100 hapo ndio Engineering ilipolala”
“Sasa tunashangaa baadhi ya Watu wanahoji kuhusu body ooh gari la kizamani sijui taa imekaaje, ukishatengeneza gari ikatembea unaweza kuweka body na namna yoyote unayotaka, tumepokea maoni yao na mapungufu mengine wamesema in positive way lakini tumeyapokea yote”
“Tuwaambie tu kwamba hili bado sio gari, ni prototype, golf car ambayo ipo silence, inaweza kutumika kwenye Airport, Mahoteli makubwa kuwazungusha Watalii, sio gari ya kusafiri Mkoa mmoja kwenda Mkoa mwingine, kila kitu tumetengeneza wenyewe, tuna mpaka invoice ya wapi tumenunua vyuma, springs n.k vingi tumenunua ndani ya Nchi lakini vingine vichache tumenunua nje kwakuwa ndani hakuna mfano taa na tairi”
PLAY: WATANZANIA WABUNI GARI INAYOTUMIA UMEME UDSM “TUMEANZA KUUNDA GARI YA POLISI AMBULANCE ITAFATA”