Kampuni kubwa ya utengenezaji wa magari aina ya Ambassador ya nchini India imefunga huduma zake za uzalishaji kwa madai ya kugubikwa na madeni na kukosekana na mahitaji ya ya gari hilo ambalo liliuzwa sana na kuweka matabaka katika nchi hiyo kutokana na gharama zake.
Kiwanda hicho cha Hindustan ambacho ni cha zamani zaidi kuliko vyote nchini humo imefunga huduma zake katika Jimbo la Uttarpara Magharibi mwa Bengal ambako imekuwa ikitengeneza magari ya aina hiyo tangu mwaka 1957.
Afisa mkuu wa kiwanda hicho amesema kuwa kazi katika katika kiwanda hicho zimesitishwa na wamefanya hivyo kuhakikisha kiwanda hicho hakitumii fedha zaidi na kuwafanya kuweka mipango mipya ya kukirudisha.
Ungependa taarifa kama hizi zikufikia haraka na kwa wakati?, niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.