Mahakama ya Uhispania hivi majuzi iliamua kwamba kampuni ya umeme imlipe mfanyakazi wake waliomsimamisha kimakosa ambaye ni mmoja wa mafundi wao wa umeme kwa kunywa bia kazini tukio ambalo hawakuweza kulidhibitisha kuwa alikuwa amelewa.
Ijapokuwa unywaji pombe kazini huonekana kuwa sababu ya mwajiri kumfukuza mfanyakazi, maofisa wa mahakama huko Hispania, waliamua hivi majuzi kwamba hilo linatumika tu wakati mwajiri anaweza kuthibitisha kwamba mfanyakazi wake alikuwa amelewa.
Kulingana na Oddity Central, fundi umeme alikuwa amelewa sana hadi hakuweza tena kutekeleza majukumu yake kwa usalama na alifutwa kazi mnamo Septemba 2021 baada ya kuwa na kampuni hiyo kwa miaka 25.
Hivi majuzi, mahakama iliamuru kampuni hiyo imlipe ($52,000) sawa na Tsh 122,200,000 kwa kushindwa kuthibitisha kwamba alikuwa amelewa au hawezi kutekeleza majukumu yoyote na zaidi ya hayo, walishindwa kuzingatia majira ya joto, ambayo yaliripotiwa kuhalalisha unywaji wapombe kwa fundi umeme.
Fundi huyo wa umeme alifutwa kazi baada ya mpelelezi wa kibinafsi kudai kukusanya ushahidi kwamba alikuwa akinywa pombe kazini kwa wiki kadhaa na kusema aliripotiwa kunywa kiasi kikubwa cha pombe kutwa nzima na katika barua yake ya kusitishwa, kampuni hiyo ilisema mwanamume huyo na wenzake walionekana wakiacha kunywa kwenye baa hiyo mwendo wa saa 8:27 asubuhi na walinunua chupa nyingine nne za bia wakati wa chakula chao na alasiri Baadaye alasiri hiyo hiyo alikunywa chupa nyingine pamoja na jioni hiyo karibu 6:30 p.m.
Zaidi ya hayo, mpelelezi huyo wa kibinafsi alisema walimwona fundi huyo wa umeme na wenzake wakinywa lita saba za bia kati ya asubuhi na mwisho wa mapumziko yao ya chakula cha mchana.
Hata hivyo, mahakama haikukubaliana na ushahidi huo na kusema kuwa mpelelezi huyo alishindwa kutaja iwapo mfanyakazi huyo alikuwa amelewa kiasi cha kushindwa kufanya kazi.
Kusimamishwa kazi kwa ghafla kunafafanuliwa nchini Uhispania kuwa ni wakati mwajiri anakatisha mkataba wa ajira bila sababu za msingi au bila kukamilisha michakato ya kisheria inayohitajika,mkataba wa wafanyakazi wa Uhispania (Estatuto de los Trabajadores) unabainisha masharti ambayo kusimamishwa kazi kutachukuliwa kuwa si ya haki hii ni pamoja na ukiukaji wa mkataba, ubaguzi, ugonjwa na kulipiza kisasi.