Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Comred Daud Yassin amezindua Kamati ya Uchumi, Fedha na Uwezeshaji yenye wajumbe saba walioteuliwa na uongozi wa UVCCM Mkoa wa Iringa.
Uzinduzi wa kamati hiyo umefanyika Alhamisi, Aprili 27, 2023 katika Ofisi za CCM Mkoa wa Iringa.
Akitoa hotuba fupi kwenye uzinduzi huo, Mwenyekiti Yassin amewapongeza wajumbe walioteuliwa na kwamba anayo imani kubwa kwamba watatekeleza majukumu muhimu yahusuyo uchumi kwenye jumuiya hiyo.
Mwenyekiti Yassin amesema suala la kuimarisha uchumi kwenye chama na jumuiya zake ni ajenda muhimu kwa wakati huu.
Kutokana na hilo, amewataka viongozi wa UVCCM washirikiane vyema na kamati hiyo kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ahmed Abri (Asas) ameshukuru kwa niaba ya wajumbe wa Kamati hiyo, huku akitoa ahadi kwamba watajitahidi kuhakikisha UVCCM Mkoa wa Iringa inajiimarika kiuchumi kupitia miradi mbalimbali.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa Ndugu Agrey Tonga amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa
Daud Yassin kwa kukubali kufika kuzindua kamati hiyo.
Amemuahidi Mwenyekiti wa CCM Mkoa kwamba kwamba watahakikisha suala la uchumi kwenye Jumuiya hiyo linafanikiwa ktk kipindi chake cha uongozi.