Promota wa pambano la kati ya bondia mtanzania Hassan Mwakinyo na Kuvesa Katembo kutoka nchini Afrika Kusini ambalo lililofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma amezungumzia suala la mkataba baada ya Bondia Ibrahim Mwakalebela aliyefariki duniavsiku chache baada ya pambano hilo
Mwakalebela alishindwa kuendelea na pambano katika round ya tatu na kuanguka wakati akipigana na Laurent Segubo “SEGU Jr”na kukimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na siku ya pili alionekana kupata shida eneo la kichwani na kutakiwa kufanyiwa upasuaji
“Mkataba ukimalizana kwenye ulingo bondia anaenda na promota anaenda mkataba unaishia hapo na ndio wajibu nilionao na suala kama hili halijawahi kutokea na tuanzie hapa baada ya kutokea”- Promota Lady in Red Promotion Sophia Mwakagenda