Jopo la wataalam wa afya duniani watakutana Alhamisi ili kuamua ikiwa COVID-19 bado ni dharura chini ya sheria za Shirika la Afya Ulimwenguni, hali ambayo inasaidia kudumisha umakini wa kimataifa juu ya janga hilo.
WHO kwa mara ya kwanza ilipatia mlipuko wa janga Ła Covid pamoja na tahadhari mnamo Januari 30, 2020, na jopo limeendelea kutumia lebo hiyo tangu wakati huo, kwenye mikutano inayofanywa kila baada ya miezi mitatu.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema anatumai kumaliza dharura ya kimataifa mwaka huu kwani bado hakuna makubaliano ya njia ipi bora ambayo inaweza kuondoa tishio la mlipuko ambayo jopo linaweza kuwapatia washauri wa WHO na wataalam mpaka sasa waliambia shirika la habari la Reuters.
“Inawezekana kwamba dharura inaweza kumalizika, lakini ni muhimu kuwasiliana kwamba Covid bado ni changamoto ngumu ya afya ya umma,” alisema Profesa Marion Koopmans, daktari wa virusi wa Uholanzi ambaye yuko kwenye jopo la WHO. Alikataa kubashiri zaidi kabla ya majadiliano, ambayo ni ya siri.
“Dharura zote lazima zifikie mwisho baada ya kujadiliana kwa wataalam,” Lawrence Gostin, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Georgetown nchini Marekani
Karim, ambaye hayumo kwenye jopo la WHO, alisema ikiwa hali ya dharura itaondolewa, serikali zinapaswa kudumisha mipango ya upimaji, chanjo na matibabu.