Mhubiri mwenye utata wa kanisa la Good News International lililopo kaunti ya Kilifi Malindi,Kenya na mkewe Rhoda Mackenzie pamoja na na watuhumiwa wengine 16 wamefikishwa katika mahakama ya Shanzu.
Mhubiri huyo na wafuasi wake wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya ugaidi baada ya mahakama ya Malindi Kaunti ya Kilifi kuwawachilia huru na kisha kukamatwa tena
Kulingana na taarifa ni kuwa kufikia sasa Mackenzie anahusishwa na vifo vya watu takribani 100 .
Uchunguzi wa miili ya watu hao umebaini kuwa huku njaa ikionekana kuwa chanzo kikuu cha vifo, baadhi ya wahasiriwa wakiwemo watoto walinyongwa, kupigwa, au kukosa hewa.
Waendesha mashtaka wanaomba kumshikilia Mackenzie, ambaye alianzisha Kanisa la Good News International Church mwaka wa 2003, kwa siku nyingine 90 hadi uchunguzi utakapokamilika.
Hapo jana Ezekiel Odero,mhubiri maarufu wa televisheni New Life International lililopo Mavueni Kaunti ya Kilifi, , aliachiwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni 1.5 .Odero pia atakuwa akisubiri rufa aliyoikata ya kutaka huduma za Kanisa lake zilizozuiliwa ziweze kuendelea na Serikali iondoe zuio la akaunti zake za Benki ilizozifunga..
Awali, upande wa Mashitaka uliiomba Mahakama indelee kumshikilia Mchungaji huyo kwa siku 30 zaidi, ukidai unaendela kukamilisha upelelezi dhidi ya mtuhumiwa na kwamba uwepo wake nje unaweza kuharibu ushahid