Raia wa Uingereza ambaye alirejeshwa New York kutoka Uhispania mwezi uliopita amekiri makosa ya udukuzi mtandaoni na udukuzi wa kompyuta, ikiwa ni pamoja na udukuzi wa 2020 wa tovuti ya kijamii ya Twitter, Idara ya Haki ya Marekani ilisema Jumanne.
Joseph James O’Connor, 23, alishtakiwa katika Dakota Kaskazini na New York. Kesi ya Dakota Kaskazini ilihamishiwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Marekani kwa Wilaya ya Kusini ya New York.
O’Connor alikiri mashtaka yakiwemo kula njama ya kufanya ulaghai wa kutakatisha fedha kwa kutumia komputa yake .
O’Connor, ambaye alirejeshwa Marekani mnamo Aprili 26, pia atapoteza zaidi ya $794,000 sawa na zaidi ya Tsh bill.1 na kulipa fidia kwa waathiriwa, waendesha mashtaka walisema anakabiliwa na kifungo cha miaka 77 jela kwa hukumu ya Juni 23.
“Vitendo vya uhalifu vya O’Connor vilikuwa vya wazi na vya nia mbaya, na mwenendo wake uliathiri maisha ya watu wengi. Aliwanyanyasa, kuwatishia, na kuwanyang’anya wahasiriwa wake, na kusababisha madhara makubwa ya kihisia,” Msaidizi wa Mwanasheria Mkuu Kenneth Polite alisema katika taarifa.
Waendesha mashitaka walisema mipango hiyo ni pamoja na kupata ufikiaji usioidhinishwa wa akaunti za mitandao ya kijamii kwenye Twitter mnamo Julai 2020 na pia akaunti ya TikTok mnamo Agosti 2020. Pamoja na washirika wake waliokula njama, O’Connor aliiba angalau $794,000 ya pesa taslimu.
Shambulio la Twitter la Julai 2020 lilikamata akaunti mbalimbali zilizothibitishwa, zikiwemo za mgombea urais wa wakati huo wa Demokrasia Joe Biden na Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla Elon Musk, ambaye sasa anamiliki Twitter.