Imeelezwa kwamba Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dr.Tulia Ackson ameonyesha nia ya kugombea kiti cha Urais wa Uspika wa Bunge la Dunia IPU.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mbunge wa Singida Mashariki, Elibariki Kingu amesema;
“Safari hii ni zamu ya Afrika, urais huo wa bunge la Dunia inakuwa ni mzunguko kila bara linapewa nafasi ya kuongoza kwa miaka mitatu hivi sasa hivi tunavyozungumza Rais aliyepo madarakani anatokea Ureno na muda wake unaelekea kuishal, nafasi hii ni muhimu kwa nchi kwa sababu Rais wa Bunge la Dunia anakuwa na mfano mkubwa sana katika taasisi zile za dunia kwa maana UN na mashirika mbalimbali ya kidunia,”.
Endapo Dr.Tulia akishika nafasi hii kwanza tutakuwa tumelitangaza taifa letu, tutakuwa tunaendelea kuiinua Diplomasia ambayo Rais wetu na Waziri wamekuwa wakiitangaza,”.