Ukosefu wa Mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi wa vyuo imekuwa ni changamoto kubwa na kupelekea wahitimu wanapokuwa kazini kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha Baraza la taifa la Elimu ya Ufundi na mafunzo ya Ufundi STADI NACTIVET kwa kushirikiana na chama cha waajiri Tanzania pamoja na washirika wa maendeleo kwa kuliona hilo wamekutana ili kupanga mikakati mbalimbali kuhusu utoaji wa mafunzo kwa vitendo.
Katika Mkutano huo Prof. Joyce Ndalichako Waziri wa Kazi Ajira Vijana na Watu wenye ulemavu ambae ni Mgeni rasmi ameeleza lengo la mkutano huo ni kuhimalisha Elimu ya Ufundi stadi kwa kwa wanafunzi wa vyuo vya kati ili kukuza soko la ajira kwa vijana.
Pia itasaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa waajiri yakuwa wanafunzi wanapotoka vyuoni wanakuwa hawana ujuzi wa vitendo wa vitu wanavyosemea na kusababisha kushindwa kutenda kazi kwa ubora wanapokuwa kazini.
Mkutano huo umewakutanisha wageni kutoka ndani na nje ya nchi wakijadili mada mbalimbali zitakazo wezesha mafunzo ya ujenzi wa ujuzi wa vitendo ili kuwajengea uwezo wanafunzi wanapokuwa vyuoni Dr Adolf Rutayuga katibu mtendaji baraza la taifa la Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET)
Prof Edda Tandi kaimu Mkuu wa chuo cha biashara CBE na Masozi Nyirenda Kaimu Mkurugenzi wa utafutaji rasilimali na miradi (TEA) ni Baadhi ya Washiriki wanasema mafunzo kwa vitendo ni muhimu sana kwa vijana Kwani itawasadia kujikimu katika maisha yao wanapokuwa kazini.