Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki Mkutano wa 15 wa Maspika wa Mabunge ya Nchi Jumuiya za Afrika Mashariki (EAC Speakers’ Bureau) uliofanyika katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha leo Mei 19, 2023.
Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamekubaliana kupitishwa kwa sheria ya kuanzishwa kwa Jukwaa la pamoja na umuhimu wa kulifanya kuwa moja ya Taasisi rasmi za Jumuiya ya Afrika Mashariki