Mkutano Mkuu wa 7 wa ID4Africa Augmented General (AGM) umezileta pamoja serikali, washirika wa maendeleo na wabunifu katika mkuktano huo wa Nairobi ili kutathmini jinsi utambulisho wa kidijitali unavyoweza kusaidia katika masuala ya usalama na kulinda heshima za watu na kurahisisha huduma kwa raia.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Julius Bitok, Katibu Mkuu katika Idara ya Taifa ya Uhamiaji na Huduma kwa Raia nchini Kenya, amesema kuwa, Kenya kwa sasa iko katikati ya mchakato wa kubadilisha vitambulisho vya taifa vya kidijitali kutoka kitambulisho cha kizazi cha pili hadi cha tatu.
Bitok alisema pia hiyo jana Jumanne kuwa, mfumo unaotegemewa katika vitambulisho hivyo vipya vya kidijitali utaipa serikali takwimu za kuaminika na kuisaidia sana kuwafikisha wananchi huduma kwa urahisi zaidi.
Wakati wa hafla hiyo, ID4Afica pia itaandaa onyesho la teknolojia ya kitambulisho na suluhisho na zaidi ya waonyeshaji 100.
Katika taarifa ya hivi majuzi, Mwenyekiti Mtendaji wa ID4Africa Dkt. Joseph Atick alisema idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura inaangazia mahitaji makubwa ya kimataifa ya utambulisho wa kidijitali.
“Maisha yetu yanapozidi kusonga mtandaoni, kujithibitisha kidijitali kumekuwa muhimu kwa kupata huduma muhimu, kushiriki katika shughuli za kiuchumi, na kutumia haki na uhuru wetu.” alisema.
Utambuzi umekuwa nguzo katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika miaka ya hivi karibuni bado Waafrika wengi hawana utambulisho wa kisheria au kidijitali jambo ambalo anadai kuwa linakwamisha ushiriki wao kamili katika jamii ikizingatiwa umuhimu wa tukio hilo.