Wazazi weshauriwa kuwapelekea vijana wao kwenye shule za Ibun Jazar kwani shule hizo ni za Kiislam na zenye malengo yakutoa elimu yenye maadili mema.
Mkurugenzi wa Shule hizo Sheikh Othman Ali Kaporo alisemaJijini Dar es Salaam hivi karibuni kuwa shule hizo malengo yakeni kutoa elimu bora kwa vijana inayoambatana na maadili mema.
“Shule hizi zina mlengo ya kuwalea watoto katika maadilimema kupitia a kitabu cha Quran tukufu na hivyo basizimeweza kutoa vijana wengi wenye maadili mema na wakatihuo huo wakiwa na kiwango cha elimu chenye kuridhisha,” anasema.
Anasema kuwa mafanikio yote hayo yametokana na juhudi zawatendaji wakuu wa taasisi wakiwamo walimu wakuu,mameneja wa shule za Ibun Jazar katika kufikisha ujumbe naelimu bora kwa vijana.
“Ibun Jazar ni miongoni mwa watu wanaochangia kuzalishanguvu kazi imara , ulimwengu hivi sasa unalia na vitu sanamiongoni mwavyo ni watu kupokea rushwa katika baadhi yataasisi,” anasema .
Kutokana na hilo anasema taasisi yake inale vijana nakuwafundisha kuwa rushwa ni adui wa haki na ni dhambi mbeleya Mwenye zi Mungu kutoa au kupokea rushwa .
Anafafanua kuwa ,malezi haya ya kiroho na kiimani ndiyo vitupekee vinavyoweza kuisaidia jamii kuwa na maadili memahivyo naiomba jamii tushirikiane ili kujenga jamii bora yaKitanzania.
Naye na Meneja wa Shule ya Sekondari ya Ibun Jazar Mtoto Bakari anasema kuwa shule hizo vijana wanahifadhi Qurantukufu , wanafundishwa elimu ya dini na masomo ya kawaida .
“Kikubwa ambacho tunaomba umma ufahamu ni kwambatunawafundisha vijana kuwa na maadili mema ili wanapotokahapa kwenda kulitumikia taifa wawe ni vijana wenye maadilimema kwa taifa lao,”
Anasema pia kuwa utafiti umeonyesha kuwa vijanaanapofundishwa kuhifadhi Quran tukufu basi hata uwezo wake wa kuelewa masomo mengine unakuwa mkubwa.
Shule ya Msingi Ibun Jazar na Sekondari zipo Vikindu WilayaMkuranga Mkoa wa Pwani na hadi sasa zimeshasomesha vijanawengi ambao wamemaliza vyuo vikuu mbalimbali na kwa sasataasisi hiyo inasomesha vijana wengine katika vyuo vikuumbalimbali .
Akizungumzia matokeo ya mwaka jana kidato cha nne anasemakatika watahiniwa 69 , waliofaulu kwa daraja la kwanza walikuwa 58 na daraja la pili 11.