Ni Mei 29, 2023 ambapo kumefanyika Maonesho ya Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT).
Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa kimataifa AICC Mkoani Arusha, Huku Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas, Ahmed akiwa ni miongoni waliopata nafasi ya kuweka bidhaa zao katika maonesho hayo.
‘Ndugu mgeni rasmi tunashukuru uongozi wa ALAT kwa kutupa fursa hii ya kuwa miongoni mwa wadhamini lakini nje ya hapo tumekuwa wadau wa karibu sana wa halmashauri ya vijiji na Manispaa’- Ahmed Asas
‘Na katika sekta yetu ya Asas tumekuwa tukiupa kipaumbele masuala ya Afya na niseme ndio kampuni ya kwanza kuanzisha mradi wa ‘maziwa mashule’ ambapo mpaka sasa tunauwezo wa kuzalisha maziwa Elfu sita kwa mwezi na huduma hii tunaitoka katika shule 11′- Ahmed Asas
‘Na Mikoa ambayo tunatoa huduma hii ni Mbeya, Njomba na Iringa lakini Mheshimiwa nina wito kwa ALAT kuwakaribisha Iringa waje kujifunza na kufahamu yale ambayo ni mageni kwao na Mungu akijaalia sisi tunaweza tukawa wanyeji wao’- Ahmed Asas
Aidha katika ufunguzi huo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ambapo ametoa wito kwa viongozi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia mipaka na majukumu yao katika utendaji wa kazi ili kuepusha migogoro na miingiliano katika kuwahudumia wananchi.