Ni Mei 30, 2023 ambapo Waziri wa Nishati, January Makamba amehojiwa katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa Clouds TV kuhusu Wizara anayoitumikia.
Fahamu sentensi zake kwa kile alichozungumza leo…’Wizara hii inahusika na sekta nyeti Sana ya umeme na mafuta na gesi na sekta hii ndio mhimili wa uchumi wa nchi yetu. Bila utulivu katika biashara ya mafuta wa upatikanaji na wa bei mambo hayaendi. Mmetoka Dar es Salaam nimefika hapa Dodoma kutokana na chombo mlichokitumia linatimia mafuta iwe ni ndege au usafiri barabarani kama mmetumia treni nayo unatumia umeme kwahiyo utaona sekta yetu ndio inasimamia uchumi” Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba
“Tumepiga hatua kubwa katika mambo ambayo tulitaka kuyafanya lakini kwa binafsi sijafika pale nilipokuwa napatamani katika mabadiliko na maboresho ambayo yanapaswa kufanyika. Tumebadilisha utamaduni wa kazi katika Wizara yetu kuna uwazi zaidi, ukweli kuhusu mambo yanavyoendelea”- Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba
Tunamshukuru Sana Rais Samia Suluhu Hassan ametupatia sapoti kubwa ya bajeti lakini miongozo maelekezo, uwelewa inapotokea changamoto na ametupatia muda ambao umetupa utulivu wa kufanya kazi hizi”– Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba
“Dhamira yetu Sisi kama wizara na kesho tutasema ni kuendelea kuhakikisha kwamba sekta ya nishati inashamilisha maendeleo ya nchi yetu na ustawi wa Watanzania. Kuna maboresho ndani ya miaka Miwili suala la changamoto ya umeme litakuwa historia hapa nchini”- Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba
‘Watu wanalalamika kukatika umeme Rais Samia ametupatia Trilion 1.9 ya kufanya miradi 26 na miradi hio imeanza, bei ya mafuta imeshuka. Tumezima tayari baadhi ya maeneo yaliyokua yanazalisha umeme wa Dizeli’- Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba
“Tunafahamu kwamba kihistoria tumekuwa tukitegemea maji kuzalisha umeme na tumekuwa katika changamoto kwa sababu wakati wa ukame muda wote vyanzo vinakuwa vinakauka. Tunachofanya sasa hivi kuongeza vyanzo vingine na kupunguza utegemezi wa maji ili kuondoka na risk inayotokana na mabadiliko ya tabia nchi pia na kuwa na gridi ambayo ni imara” Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba
Tunaingiza umeme wa upepo mwakani, najua hii italeta mjadala lakini tutaingiza umeme wa makaa ya mawe mwaka 2025, na tutaingiza sasa umeme wa joto ardhi” Waziri January Makamba akieleza kuhusu mipango ya Serikali kutumia vyanzo vingi vya nishati”– Waziri wa Nishati Mhe.January Makamba
Aidha Amesisitiza kwamba Tanzania itatumia vyanzo vyote vya asili ilivyobarikiwa kuzalisha umeme.