Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameidhinisha sheria ya kukomesha wizi wa viungo na tishu za binadamu, waziri wake wa afya alisema Jumanne, katika taifa ambalo wanawake wameripotiwa kulaghaiwa kufanyiwa upasuaji usio wa lazima.
Vyombo vya habari vya nchini katika miaka ya hivi karibuni vimeripoti kesi za wanawake walioajiriwa kufanya kazi za nyumbani katika Mashariki ya Kati wakiwekwa katika taratibu za matibabu ambapo figo zao zinauzwa katika mitandao ya kimataifa ya biashara haramu.
Katika ujumbe wake wa Twitter, Waziri wa Afya Jane Aceng alimshukuru Museveni kwa kutia saini Mswada wa Uchangiaji na Upandikizaji wa Kiungo cha Binadamu Uganda 2023 ili kudhibiti vyema eneo hilo. “Mlango sasa uko wazi kwa #Uganda kuanza sura mpya ya Kupandikiza Kiungo,” alisema.
Hayo yanajiri siku moja baada ya Museveni na serikali yake kulaaniwa na kimataifa kwa kutunga mojawapo ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya LGBTQ, ambayo ni pamoja na hukumu ya kifo kwa “ushoga uliokithiri”.
Sheria ya uchangiaji na upandikizaji, ya kwanza ya aina yake nchini Uganda, inakataza shughuli zozote za kibiashara katika viungo vya binadamu na tishu. Adhabu ni pamoja na kifungo cha maisha na faini kali.
Mnamo Septemba 2022, Aceng alikiri kwamba mahitaji ya upandikizaji wa viungo nchini yalikuwa juu, lakini hakukuwa na sheria.