UNDP Tanzania, kupitia proramu yake ya FUNGUO, imefungua dirisha la pili la udhamini kwa kampuni changa za kibunifu za Kitanzania. FUNGUO inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na Serekali ya Uingereza, imetangaza kutoa ufadhili wenye thamani ya shilingi bilioni moja ili kuchangia katika uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Kwa kuzingatia jitihada za makusudi za kuhamasisha na kukuza wanawake wabunifu na wajasiriamali, FUNGUO imetenga asilimia 30 ya fedha zilizopo katika dirisha hili kwa ajili ya kampuni changa zinazomilikiwa kwa kiasi kikubwa na wanawake.
FUNGUO inalenga kuongeza idadi ya kampuni changa za kibunifu zinazofanikiwa kuvutia uwekezaji ili zikue na kuzalisha ajira kwa vijana, kuchangia pato la taifa na kuchangia katika uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Tangu dirisha la kwanza lililozinduliwa mwezi wa sita mwaka jana, FUNGUO imeweza kufadhili kundi la kwanza la kampuni 26 zinazotarajia kuzalisha au kudumisha ajira zisizopungua 2300 kwa vijana wa kike na wa kiume ifikapo mwaka 2024. Matokeo ya ufadhili huu yamekuwa ya kipekee kwa baadhi ya kampuni zilizonufaika. Baadhi ya mafanikio haya ni pamoja na kampuni mbili zilizoaminiwa na serikali na kushinda zabuni zenye thamani ya karibu TZS 6 bilioni ili kutekeleza miradi ya kuendeleza sekta ya uvuvi. Kampuni zingine 2 zilifanikiwa kupata wawekezaji wengine, na hii inadhihirisha jinsi programu ya FUNGUO ilivyoweza kuwafungulia njia.
Katika wasilisho lake kwenye uzinduzi huu, Meneja wa Programu, Joseph Manirakiza aligusia mchango wa programu hii kwa upande wa mazingira ya kibiashara “Hapa, FUNGUO ilichangia katika kutunga Mwongozo wa Kwanza wa Kitaifa wa Uchangishaji Fedha (Crowdfunding Guidelines) kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Uwekezaji (CMSA). Mwongozo huu ukisha kamilika hivi karibuni utafungua fursa nyingi kwa kampuni changa kuweza kuchangisha mitaji midogo midogo kutoka kwenye jamii.”
““Mafanikio ya FUNGUO katika awamu ya kwanza ya ufadhili ni ushahidi tosha wa vipaji na ubunifu usio na kifani uliopo katika mfumo wa kampuni changa hapa nchini,” alisema Bw. Cedric Merel, Mkuu wa Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya. “Tunafurahi kuwa sehemu ya kuwawezesha wabunifu na tunatarajia kuona ukuaji endelevu na michango chanya itakayoletwa na kampuni hizi katika jamii na katika uchumi wa nchi kwa ujumla.”
“Hili dirisha la pili la Maombi ya Ufadhili chini ya Programu ya Ubunifu ya FUNGUO ni ishara nyingine ya dhamira ya UNDP ya kukuza ubunifu na kufanikisha malengo ya maendeleo ya kitaifa,” alisema Bi. Christine Musisi, Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania. “Tunaamini katika nguvu ya vijana wengi wabunifu ambao wamejitolea kuleta mabadiliko kupitia kuanzisha biashara. Hii si tu inatengeza ajira kwa vijana wao na wenzao, lakini pia inachangia maendeleo endelevu ya nchi yao. UNDP inaendelea kuwasaidia kupitia mipango kama FUNGUO na mingineyo, kwa kushirikiana na wahisani wetu kama EU na Serikali ya Uingereza. Tunaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kufanya kazi kwa karibu sana na wadau wa maendeleo, ili kuwawezesha kuchangia ipasavyo katika kuendeleza vijana wenye bidii ya kutengeneza kesho yao iliyo bora.”
Ivana Damjanov, Msimamizi wa Programu ya Uchumi Jumuishi wa Kidijitali, UNCDF, alisema, “Kuunga mkonoprogramu ya FUNGUO kunasaidia kufanikisha lengo letu la pamoja la kukuza maendeleo ya kiuchumi na kuhamasishaubunifu nchini Tanzania. Kwa upande mwingine, chini ya mradi wa Digital4Tanzania Tanzania-Inclusive Digital Economy (D4T-TIDE) uliofadhiliwa na EU, tunajitahidi kuendeleza mfumo wa ubunifu na kuihamasisha mtaji kwa ajili ya ukuaji wao. Tuko pamoja katika kutumia uwezo wa uchumi wa dijitali wa Tanzania, kuimarisha kampuni za fintech na biashara za mtandaoni, kukuza ukuaji wa kiuchumi, na kuzalisha ufahamu utakaoaosaidia kuongeza kasi ya mabadiliko ya kidijitali.”