Bunge la Zimbabwe limepiga kura kuunga mkono mswada wenye utata wa kuwaadhibu raia kwa “vitendo visivyo vya kizalendo”, ikiwa ni pamoja na kuwatoza faini kubwa au hata adhabu ya kifo huku wakosoaji wakiita siku ya giza kwa demokrasia.
Kipengele kinachojulikana kama uzalendo wa Sheria ya Jinai kinalenga wale wanaodhuru “maslahi ya kitaifa ya Zimbabwe”.
Inajumuisha raia yeyote anayekutana na mwakilishi wa nchi ya kigeni kwa lengo la kuhimiza vikwazo dhidi ya Zimbabwe au kupindua serikali.
Mswada huo unaojulikana kama kifungu cha uzalendo cha Sheria ya Jinai kinalenga wale wanaodhuru “maslahi ya kitaifa ya Zimbabwe”.
Maafisa wengi waandamizi wa serikali na makampuni yanayomilikiwa na serikali wako chini ya vikwazo vya Magharibi kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu,
Kwa muda mrefu wamelaumu upinzani kwa hili na wanataka kusitisha mikutano kati ya upinzani na maafisa wa kigeni.
Bunge lilipiga kura 99 kwa 17 kuunga mkono sheria hiyo – mojawapo ya utata mkubwa wa urais wa Emmerson Mnangagwa.
Mabadiliko hayo yenye utata yalipitishwa kama sehemu ya mfululizo wa marekebisho ya Sheria ya Jinai.
Wabunge pia walipiga kura kuunga mkono hukumu za kima cha chini kwa ubakaji.